Loe raamatut: «Nyumbani»

Font:

Kitabu kutoka LS MORGAN

Picha ya Jalada: Odile Silva Dias

Mtafsiri: Kennedy Cheruyot Langat

Hii ni hadithi ya kubuni. Lengo lake ni kuburudisha watu.

Majina, wahusika, mahali na hafla zilizoelezewa ni matokeo ya mawazo ya mwandishi.

Iwapo hali yoyote inafanana na mambo haya ni kwa bahati mbaya.

© 2021 - LS MORGAN

HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA

Ni marufuku kuhifadhi na / au kuchapisha tena sehemu yoyote ya kazi hii, kwa njia yoyote - inayoonekana au isiyoonekana - bila idhini iliyoandikwa kutoka kwa mwandishi.

Ukiukaji wa haki za kipekee za mwenye hakimiliki zitasababisha adhabu za jinai.

Hadithi fupi iliyoandikwa na LS Morgan

***

Hadithi inayovutia na ya kushangaza, ambayo inatuongoza kwa hisia za kina na maswali ya thamani. Maumivu, na upotevu wa msichana mmoja wa miaka 8 aliyekuwa anaishi na hisia za kindani, na tunachukuliwa kwa safari kurudi kwenye kumbukumbu zake hadi mahali pa kumbukumbu zake zenye uchungu lakini pia za upendo: nyumbani kwake.

Nyumbani

Kupitia uwanda wenye majani, mbali na eneo la wazi la nyasi na vichaka vilivyo kijani kibichi kila wakati kwenye mchanga mwekundu uliobanwa na maua ya dandelioni, ambayo yanarusha mbegu zao kwa upepo, mbali zaidi ya vivuli vikubwa vya miti yenye majani mengi na matunda yaliyoiva na sauti za wimbo wa ndege, papo hapo kulikuwa na nyumba. Haikuwa nyumba tu. Ilikuwa nyumbani. Aina ya nyumbani ambayo tunahisi upendo unanukia kama mkate wa mahindi uliookwa mapema asubuhi na sakafu ya saruji isiyo na kifani iliyotiwa nta, ilikuwa na njia ya miguu isiyo na viatu ya mtoto aliye na furaha na jozi mbili za miguu ya mtu mzima wa kike.

Nyumba yangu, makao yangu, makazi yangu… Ninaweza kuorodhesha majina mengi ya mahali hapo niliishi wakati wa miaka minane ya kwanza ya utoto wangu na hiyo ilinyakuliwa ghafla kutoka kwangu, kwa sauti ya kilio changu kikubwa na kilio cha juu cha mtoto niliyekuwa, ambaye hakuelewa, kwa wakati huo, sababu za kulazimishwa kuondoka.

Mara nyingi, nilijikuta nikikimbia kupitia eneo lenye watu wengi, chafu na mtaa wa kutatanisha ambao niliishi. Kwenye jaribio la tatu, akiwa na umri wa miaka kumi na mbili, babu yangu alitafuta njia ya kunizuia kuondoka. Kisha nikaendelea kutazama kupitia dirisha la ghorofa ya saba, katika jiji lililojaa majengo, magari na malori yanapita kwenye barabara yenye shughuli nyingi, na kelele, kelele nyingi ilikamilisha hali hiyo ya kusikitisha na isiyo na usemi.

Tasuta katkend on lõppenud.

€2,99

Žanrid ja sildid

Vanusepiirang:
0+
Ilmumiskuupäev Litres'is:
29 juuli 2021
Objętość:
7 lk 1 illustratsioon
ISBN:
9788835425861
Õiguste omanik:
Tektime S.r.l.s.
Allalaadimise formaat:

Selle raamatuga loetakse